P.o.Box 602, Arusha Tz
Mon - Fri : 09.00 AM - 09.00 PM
+255 762 779 547
  • Posted in: 2025-08-18 03:30:46

    Click to download Tunapenda kutangaza na kukaribisha maombi ya nafasi za kujiunga na Kidato cha Kwanza mwaka 2026. Mitihani ya kujiunga (interviews) itafanyika tarehe 20/09/2025 na 11/10/2025 katika vituo vifuatavyo: Arusha (Brainy Heroes Boys’ Secondary School), Dar es Salaam (Rugwa Primary School – Gongolamboto, Simu: 0689 104 184) na Tabora (Milambo High School – Tabora Mjini, Simu: 0624 801 937). Mtihani utaanza saa mbili kamili asubuhi (08:00 am) na mwanafunzi anatakiwa kuvaa sare za shule ya msingi aliyosoma. Shule inapokea wanafunzi wa dini zote bila ubaguzi. Muhimu kukumbuka kuwa fomu ya maombi inapaswa kujazwa kwa umakini na kurejeshwa kwenye kituo ulichopokea kabla ya tarehe ya usaili. Gharama ya fomu ni Shilingi 20,000/= (Elfu Ishirini tu) na kila mlipaji anatakiwa kupewa risiti ya malipo. Fomu za maombi zinapatikana katika vituo vifuatavyo: Shuleni Brainy Heroes, Ofisi ya Vijana St. Thereza (Arusha), pamoja na Msimbazi Centre katika chumba namba 6 na chumba namba 9.

UPCOMING EVENTS

Meet Our Staff Member

We Have Great Experience Of Staff Member

No Staff List Found!